Pata taarifa kuu

AFCON: Senegal yaanza kwa ushindi mkubwa, Cameroon na Algeria zabanwa

Mabingwa watetezi Senegal, walianza vema siku ya Jumatatu kwa kuilaza Gambia 3-0, katika mechi yake ya ufunguzi, kwenye uwanja wa Charles Konan Banny  jijini  Yamoussoukro, kuwania michuano ya AFCON baina ya nchi za Afrika inayoendelea nchini Cote Dvoire.

Lamine Camara, akisherehekea baada ya kufunga mabao mawili, Januari 15 2024.
Lamine Camara, akisherehekea baada ya kufunga mabao mawili, Januari 15 2024. © AFP / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Nyota wa mchezo huo alikuwa ni Lamine Camara, aliyeifungua nchi yake mabao mawili katika dakika 52 na 86 ya mchuano huo, baada ya bao la ufunguzi kufungwa na Pape Alassane Gueye katika dakika ya nne, baada ya kupata pasi  murua kutoka kwa mshambuliaji Sadio Mane.

Ushindi huu umewapa matumaini makubwa, Simba wa Teranga kunyakua tena taji hili na kuwapa nguvu kuelekea kwenye mchuano wake pili dhidi ya Cameroon siku ya Ijumaa.

Gambia ilikwenda mechi yake ya kwanza, baada ya siku kadhaa kususia mazoezi kwa kutolipwa marupurupu yao, jambo ambalo linaripotiwa kuwaathiri kisaikolojia.

Beki za Guinea Sekou Sylla akichuana na mshambuliaji wa Cameroon  Franck Magri, Januari 15 2024 kwenye uwanja wa Charles Konan Banny  jijini  Yamoussoukro
Beki za Guinea Sekou Sylla akichuana na mshambuliaji wa Cameroon Franck Magri, Januari 15 2024 kwenye uwanja wa Charles Konan Banny jijini Yamoussoukro AFP - ISSOUF SANOGO

Katika mechi nyingine ya kundi C, Cameroon maarufu kama Simba wasiofugika, walitoka nyuma na kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Syli National ya Guinea.

Guinea ilikuwa ya kwanza kupata bao la mapema, katika daika ya 10 kupitia Mohamed Bayo, aliyeongoza safu ya ushambuliaji baada ya kukosekana kwa mchezaji wa kutegemewa, Serhou Guirassy, anayeuguza jeraha.

Nayo Algeria, mabingwa wa mwaka 2019, ilianza kwa kushindwa kupata ushindi kwenye mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Angola baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi ya kundi D.

Baghdad Bounedjah, alianza kuipa Algeria bao la ufunguzi katika dakika 18, lakini Agostinho Cristóvão Paciência maarufu kama Mabululu akaisawazishia Angola katika dakika 68 kupitia mkwaju wa penalti.

Baghdad Bounedjah baada ya kufunga bao dhidi ya Angola.
Baghdad Bounedjah baada ya kufunga bao dhidi ya Angola. AP - Themba Hadebe

Mpaka sasa Mataifa mengine ambayo yameanza kwa sare ni pamoja na Cameroon, Nigeria, Misri na Ghana.

Burkina Faso inachuana na Mauritania katika mechi nyingine ya kundi hili mjini Bouake siku ya Jumnne jioni kabla ya kupisha mechi za kundi E, kati ya Tunisia na Namibia na baadaye Afrika Kusini na Mali, mjini Korhogo.

Siku ya Jumatano, itakuwa zamu ya kundi la F, mechi ya kwanza kati ya Morocco dhidi ya Tanzania, katika uwanja wa Laurent Pokou mjini San Pëdro na baadaye DR Congo dhidi ya Zambia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.