Pata taarifa kuu

Soka: UEFA yaahirisha mechi kati ya Israel na Uswisi iliyopangwa kuchezwaTel Aviv

Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA), chombo kinachosimamia soka barani Ulaya, kimetangaza Jumapili jioni Oktoba 8 kwamba mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 kati ya Israel na Uswisi, iliyokuwa imepangwa kuchezwa siku ya Alhamisi huko Tel Aviv imeahirishwa baada ya shambulio la Hamas dhidi ya Israel.

Vikosi vya Israel vikielekea mji wa kusini wa Sderot mnamo Oktoba 8, 2023.
Vikosi vya Israel vikielekea mji wa kusini wa Sderot mnamo Oktoba 8, 2023. © AFP - RONALDO SCHEMIDT
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kuzingatia hali ya sasa ya usalama nchini Israel, UEFA imeamua kuahirisha mechi zote zilizopangwa nchini humo kwa muda wa wiki mbili zijazo. Tarehe mpya zitathibitishwa kwa wakati ufaao,” imeelezwa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Mechi za kufuzu kwa michuano ya Ulaya kwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 21 kati ya Israel na Estonia (Oktoba 12) na kati ya Israel na Ujerumani (Oktoba 17) pia zimeahirishwa, kama vile mishuano midogo ya Ulaya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 ambayo ingezikutanisha Israel, Ubelgiji, Gibraltar na Wales kuanzia Oktoba 11 hadi 17.

"UEFA inasubiri siku chache za ziada kutathmini kama mechi ya kufuzu kaika michuano ya Ulaya kati ya Kosovo na Israel inaweza kuchezwa katika tarehe iliyopangwa awali ya Oktoba 15, au kama inaweza kuahirishwa," taarifa hiyo iimeongeza. "UEFA itaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu na kuendelea kuwasiliana na timu zote zinazohusika kabla ya kufanya maamuzi juu ya tarehe mpya na mabadiliko yanayoweza kutokea kwa mechi zingine zijazo," imeongeza.

Mapigano yanaendelea siku ya Jumapili kati ya wanaharakati wa Hamas na vikosi vya Israel, siku moja baada ya kuanzishwa kwa mashambulizi ya kushtukiza ya vuguvugu la Kiislamu la Palestina dhidi ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alizungumzia vita vya "muda mrefu" dhidi ya Hamas. Kwa mujibu wa Israel, zaidi ya watu 600 wameuawa na 2,000 kujeruhiwa kwa upande wa Israel. Katika Ukanda wa Gaza, Wapalestina 370 wameuawa na wengine 2,200 kujeruhiwa kwa mujibu wa Hamas inayodhibiti eneo hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.