Pata taarifa kuu

Jesse Lingard kuondoka Nottingham Forest

NAIROBI – Kiungo wa zamani wa Manchester United na Uingereza Jesse Lingard ataondoka Nottingham Forest mwishoni baada ya  kandarasi yake kukamilika.

 Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United Jesse Lingard
Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United Jesse Lingard AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Lingard alijiunga na Forest msimu uliopita baada ya kupandishwa daraja hadi ligi ya Premia, lakini uwezo wake haujaweza kuisadia klabu hiyo kuandikisha matokeo mazuri kwenye ligi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alikataa kujiunga na West Ham, ambapo alifanya vizuri akiwa kwa mkopo kutoka United mnamo 2021 na badala yake akalenga kusaini mkataba wa mwaka mmoja na kalbu ya Forest.

Lingard alicheza mara 20 pekee katika mashindano yote kwa Forest na alitajwa miongoni mwa wachezaji 12 walioachiliwa na meneja Steve Cooper siku ya Ijumaa.

Alicheza mara nne pekee mwaka wa 2023 na sasa atatafuta klabu ya tatu ndani ya miaka mitatu.

Lingard, ambaye alipigiwa upatu kuwa nyota baada ya kuhitimu kutoka akademia ya vijana ya United, amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa za nje ya nchi katika wiki za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.