Pata taarifa kuu

Yanga yatinga fainali ya Kombe la FA

NAIROBI – Na Paulo Nzioki

Mashabiki wa Yanga ya nchini Tanzania katika mechi ya awali ya shirikisho
Mashabiki wa Yanga ya nchini Tanzania katika mechi ya awali ya shirikisho © Yanga
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Young Africans ya Tanzania, imeingia katika fainali ya kombe la shirikisho la Azam baada ya kupata ushindi wa goli moja bila ya jibu dhidi ya Singida big stars siku ya Jumapili.

Mfungaji bora wa Yanga Fiston Mayele alifunga bao katika dakika ya 83 nje kidogo ya eneo la hatari katika pambano la kusisimua lililochezwa kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Ushindi huo unamaanisha kuwa Yanga itakutana na Azam FC katika mchezo wa mwisho wa kinyang’anyiro hicho, uliopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, katikati ya mwezi Juni.

Klabu ya Young Africans ya Tanzania, imeingia katika fainali ya kombe la shirikisho la Azam
Klabu ya Young Africans ya Tanzania, imeingia katika fainali ya kombe la shirikisho la Azam © Yanga

Azam FC imefuzu kwa fainali baada ya kuiondoa Simba kwa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Nangwanda Sjjaona.Mshindi wa shindano hilo ataiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho la CAF.

Mbali na kufuzu fainali, ushindi huo pia ni kisasi kwa Yanga dhidi ya Singida Big Stars, walioitoa Yanga katika fainali ya 2018, ambapo timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani ilitolewa kwenye uwanja huo huo.

Yanga ilitawala zaidi kipindi cha kwanza cha mechi hiyo na kutengeneza nafasi nyingi za mabao lakini ikashindwa kuzibadilisha kuwa mabao.

“Nawapongeza sana wachezaji wangu kwa ushindi huo, tulifanikiwa kuamrisha mchezo kipindi cha kwanza na kipindi cha pili, lakini tulishindwa kufunga mabao mengi, lakini cha muhimu ni kushinda mchezo ambao tulifanya na wachezaji wangu. wanastahili pongezi,” alisema Kocha Mkuu wa Yanga, Nesreddine Nabi.

Klabu ya Young Africans ya Tanzania, imeingia katika fainali ya kombe la shirikisho la Azam
Klabu ya Young Africans ya Tanzania, imeingia katika fainali ya kombe la shirikisho la Azam © Yanga

Nabi alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu sana na kwamba timu ililazimika kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake muhimu kutokana na uchovu.

“Tulikutana na mchezo mgumu, ikabidi nipumzishe baadhi ya wachezaji kutokana na uchovu, lakini baada ya mechi kuonekana kumalizika kwa sare tasa, nilibadili mtindo na kufanikiwa kushinda,”alieleza kocha Nabi.

Mfungaji wa goli pekee Mayele, pia alikiri kupata upinzani mkali dhidi ya Singida Big Stars licha ya ushindi huo huku pia kiungo wa kati wa singida Deus Kaseke akimvulia kofia mshambualiaji huyo na kumtaja kama mshambuliaji bora.

"Haikuwa mechi rahisi, na sisi (Yanga) tumetoka kwenye mechi kali ya Kombe la Shirikisho Afrika, tunahitaji ushindi huu, na tunatarajia mechi nyingine ngumu dhidi ya Azam FC," alisema Mayele.

Klabu ya Young Africans ya Tanzania, imeingia katika fainali ya kombe la shirikisho la Azam
Klabu ya Young Africans ya Tanzania, imeingia katika fainali ya kombe la shirikisho la Azam © Yanga

Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Van Pluijm amewapongeza wachezaji wake kwa kufanya vyema licha ya kupoteza dhidi ya timu ngumu kwenye michuano hiyo.

Pluijm alisema walifanya makosa na kuipa Yanga nafasi ya kushinda pambano hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.