Pata taarifa kuu

DRC: Mbemba aingia kwenye fainali ya tuzo la Marc-Vivien Foe

NAIROBI – Beki wa timu ya taifa ya DRC  na klabu ya Olympique de Marseille ya Ufaransa, Chancel Mbemba ni miongoni mwa wachezaji watatu walioingia kwenye fainali ya kuwania tuzo ya Marc Vivien Foe  msimu wa 2022-23.

Raia wa DRC Chancel Mbemba ni kati ya wachezaji 3 walioingia kwenye fainali ya tuzo ya Marc-Vivien Foe
Raia wa DRC Chancel Mbemba ni kati ya wachezaji 3 walioingia kwenye fainali ya tuzo ya Marc-Vivien Foe AP - Daniel Cole
Matangazo ya kibiashara

Tuzo la Marc Vivien Foe ni tuzo ambalo hutolewa kwa mchezaji bora wa kandanda wa Afrika, anayecheza katika michuano ya Ligi ya Ufaransa.

Majina ya watatu hao yaliekwa wazi baada ya kura kupigwa kwenye orodha ya watu wa kwanza kumi na mmoja.

Jina la mshindi wa tuzo hii litajulikana Jumanne, Mei 30 baada ya waandishi wa habari wa michezo katika vituo vya France 24 na rfi kupiga kura.

Iwapo Chancel Mbemba atashinda, atakuwa Mkongomani wa pili kushinda tuzo hili baada ya Gaël Kakuta mwaka wa 2021.

Wengine waliobaki katika kinyang’anyiro mbali na mbemba:

Seko Fofana (Ivory Coast / Lenz)

Seko Fofana, nahodha wa RC Lens
Seko Fofana, nahodha wa RC Lens © AFP / DENIS CHARLET

Seko Fofana, nahodha wa RC Lens, raia wa Ivory Coast ndiye bingwa mtetezi wa tuzo hili.

Fofana mkali wa pasi na ufungaji, mwenye umri wa miaka 27 bado ameonyesha kuwa na makali msimu huu.

Terem Moffi (Nigeria / Nice)

Terem Moffi
Terem Moffi AFP - VALERY HACHE

Kiungo huyu mchezaji wa Super Eagles mwenye umri wa miaka 23 hakika alihitaji muda kuzoea, lakini hakupoteza ufanisi wake mbele ya lango.Alihamishwa kutoka Lorient hadi Nice.

Nice inakusudia kumfanya raia  huyo wa Nigeria  kuwa mmoja wa wachezaji wao mahiri na kutegea kumuuza kwa dau nono katika soko la Ulaya.

Kwa mchango wake msimu huu, ameingia katika orodha ya wapambanaji watatu kwenye tuzo la Marc Vivien Foe.

Wachezaji wote wamecheza angalau mechi 15 kwenye Ligue 1 msimu huu.

Washindi wa matoleo matano yaliyotangulia:

2022: Seko Fofana (Ivory Coast)

2021: Gaël Kakuta (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)

2020: Victor Osimhen (Nigeria)

2019: Nicolas Pépé (Ivory Coast)

2018: Karl Toko-Ekambi (Kamerun)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.