Pata taarifa kuu

Kujiondoa kwa Nadal katika Michuano ya Tenisi Madrid

NAIROBI – Jaribio la Rafael Nadal kushinda taji la 15 la French Open limeingia mashakani baada ya Mhispania huyo mkongwe kutangaza kukosekana katika mashindano ya Madrid Masters baadaye mwezi huu. 

Rafael Nadal, wa Uhispania, akicheza dhidi ya Richard Gasquet, wa Ufaransa, wakati wa nusu fainali ya mashindano ya tenisi ya U.S. Open 2013, Jumamosi, Septemba 7, 2013, New York. (Picha ya AP/David Goldman)
Rafael Nadal, wa Uhispania, akicheza dhidi ya Richard Gasquet, wa Ufaransa, wakati wa nusu fainali ya mashindano ya tenisi ya U.S. Open 2013, Jumamosi, Septemba 7, 2013, New York. (Picha ya AP/David Goldman) AP - David Goldman
Matangazo ya kibiashara

Nadal mwenye umri 36, hajacheza kwa ushindani tangu kukumbwa na tatizo kwenye misuli ya mgongo lililotatiza harakati zake wakati wa kushindwa kwake raundi ya pili na Mackenzie MacDonald kwenye michuano ya Australian Open mwezi Januari. 

"Hapo awali ilibidi niwe na kipindi cha wiki sita hadi nane cha kupona na sasa tuko na wiki ya 14," alisema Nadal kwenye mtandao wa kijamii. "Ukweli ni kwamba hali sio vile tungetarajia." 

Nadal amekosa mashindano ya Monte Carlo na Barcelona ambapo ameshinda mataji 11 na 12 mtawalia. 

Madrid imekuwa uwanja mwingine wa kuwinda mataji kwa Nadal kwa miaka mingi akishinda mataji matano kwenye Caja Magica. 

"Hakuna kingine cha kufanya zaidi ya kujaribu kuwa na mtazamo mzuri kwa muda wote huu," Nadal aliongeza. "Ili kujaribu kujipa nafasi ya kushindana katika baadhi ya mashindano ya msimu ambayo yamesalia na hakuna suluhisho lingine zaidi ya kufanya kazi na kuwa na mawazo mazuri." 

Mjini Barcelona siku ya Alhamisi, mchezaji wa pili Stefanos Tsitsipas alitinga hatua ya nane bora kwa ushindi wa seti moja kwa moja dhidi ya Denis Shapovalov. 

Mgiriki huyo mwenye umri wa miaka 25 atacheza mchezaji wa nane Alex de Minaur. Kulikuwa na ushindi pia kwa Alejandro Davidovich Fokina pamoja na mchezaji wa nne Jannik Sinner. 

Ripoti yake mwanaspoti wa RFI Kiswahili, Paul Nzioki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.