Pata taarifa kuu

Inter Milan yashutumu kufungiwa kwa Lukaku

NAIROBI – Inter Milan imeshutumu kupigwa marufuku kwa mshambuliaji Romelu Lukaku katika nusu fainali ya Kombe la Italia.  

Romelu Lukaku wa Inter Milan
Romelu Lukaku wa Inter Milan POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Inter Milan Lukaku ni mwathiriwa wa  ikisema ni unyanyasaji na ubaguzi wa rangi kwani yeye nidye mtu pekee aliyeadhibiwa baada ya Juventus kushinda rufaa ya kesi yao. 

Mahakama ya rufaa ya Shirikisho la Soka la Italia (FIGC) ilithibitisha kusimamishwa kwa Lukaku ikimaanisha kuwa hataweza kushiriki katika nusu fainali ya mkondo wa pili Jumatano huko San Siro. 

Lukaku alipata adhabu hiyo baada ya kupata kadi mbili za njano, ya pili ikija baada ya kushangilia bao lake mbele ya mashabiki wa Juventus baada ya mkwaju wa penalti katika dakika za lala salama ambao uliifanya Inter kulazimishwa sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza mjini Turin. 

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji alishikilia kidole chake mdomoni kama alivyofanya baada ya kuifungia nchi yake bao na kuwaambia wafuasi wa Juve "wanyamaze". 

Siku ya Jumatano, Juventus walishinda rufaa yao walipomtaka Lukaku kufungiwa kutocheza mechi moja wakidai Lukaku aliwatusi mashabiki wao. 

Tukio la hivi punde la ubaguzi wa rangi katika uwanja wa michezo wa Italia lilizua lawama kutoka kwa Kylian Mbappe wa Ufaransa na rais wa FIFA Gianni Infantino. 

"Historia inajirudia," Lukaku aliandika kwenye Instagram baada ya tukio hilo. 

"Nilipitia mwaka 2019 ... na 2023 tena", akimaanisha miaka mitatu iliyopita, ambapo wataalam wa Inter walimwambia kwamba nyimbo za tumbili zilizoelekezwa kwake na mashabiki wa Cagliari hazikuwa za ubaguzi wa rangi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.