Pata taarifa kuu

Raia wa Tanzania Gabriel Geay amaliza wa pili katika mbio ndefu za Boston.

NAIROBI – Mwanariadha wa Tanzania Gabriel Geay amemaliza katika nafasi ya pili katika mbio ndefu za Boston Makala ya 127. 

Benson Kipruto, wa Kenya, kulia, Evans Chebet,wa Kenya, katikati,na Gabriel Geay, wa Tanzania, kulia, wakati wa mbio za  Boston Marathon awamu ya 127, Jumatatu, Aprili 17, 2023 (AP Photo/Steven Senne)
Benson Kipruto, wa Kenya, kulia, Evans Chebet,wa Kenya, katikati,na Gabriel Geay, wa Tanzania, kulia, wakati wa mbio za Boston Marathon awamu ya 127, Jumatatu, Aprili 17, 2023 (AP Photo/Steven Senne) AP - Steven Senne
Matangazo ya kibiashara

Watanzania hawajakua wakifanya vizuri katika kitengo cha riadha jambo ambalo limewafanya watanzania wengi kufurahia ushindi wa Gabriel. 

Raia huyo wa Tanzania amemaliza nyuma ya mshindi raia wa Kenya  Evans Chebet aliyetetea taji lake la Boston Marathon katika mbio hizo zilizofanyika nchini Marekani siku ya Jumatatu. 

Chebet alimshinda Gabriel Geay wa Tanzania kwa saa 2:06:04 huku Kipruto akimaliza wa tatu kwa saa 2:06:06. 

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Eliud Kipchoge alishindwa kuhimili joto na kumaliza wa sita kwa saa 2:09:23. 

Hellen Obiri, mshindi wa medali ya fedha ya Olimpiki mara mbili katika mbio za mita 5,000, alishinda kwa upande wa wanawake. 

Obiri ambaye alikua anakimbia kwa mara ya pili kwenye mbio ndefu kwa mda wa saa 2:21:38. 

"Nilijaribu kuwa mvumilivu na kungoja wakati mwafaka utimie," alisema Obiri, ambaye alimaliza katika nafasi ya sita mwaka jana mjini New York katika mbio ndefu kwa mara ya kwanza. "Leo ilikuwa wakati wangu,” aliongeza. 

Raia wa Ethiopia Amane Beriso, aliyemaliza wa tatu katika mbio ndefu za Valencia alimaliza nyuma ya Obiri kwa sekunde 12. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.