Pata taarifa kuu

FIFA kuandaa mashindano ya FATSHI CUP jijini Kinshasa

NAIROBI – Shirikisho la soka duniani FIFA, litaandaa mashindano ya kombe la FATSHI yatakayofanyika jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya kidemokrasia Congo mwezi mwaka huu . 

FIFA kuandaa mashindano ya FATSHI CUP jijini Kinshasa
FIFA kuandaa mashindano ya FATSHI CUP jijini Kinshasa © Getty Images/iStock/Artisteer
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao kilichofanyika hapo jana Jumatatu Aprili 17 mjini Kinshasa, waziri wa michezo, Kabulo Mwana Kabulo, amedhibitisha taarifa hiyo. 

Waziri kabulo aliwaeleza wajumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka la DRC (FECOFA) kwamba nchi hiyo itafadhiliwa na FIFA. 

Mashindano haya yanalenga kuongeza hali ya ushindani katika timu za taifa za U20 za ukanda wa Afrika ya Kati zinapopambana katika mashindano makubwa ya vijana kama Kombe la Dunia. 

Katibu mkuu wa FECOFA Belgian Situatala Matuluakila katika mawasiliano na Wizara ya Michezo amesema pia Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeunga mkono mashindano hayo ambayo yanaandaliwa kwa mara ya kwanza. 

"Kufikia Ijumaa hii, tutaelekea Brazzaville kukutana na rais wa UNIFFAC Guy Moyalas na rais wa FECOFOOT kujadili kuhusu mashindano haya," ameelezea Belgian Situatala. 

DRC itashiriki na uteuzi wake wa Leopards U20 ukiongozwa na Michel Dinzey. 

Wateule wengine sita wa vijana wa UNIFFAC, ikiwa ni pamoja na Kongo na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, washindi wa mwisho wa CAN U20 Misri mwaka 2023, watacheza na DRC. 

Mashindano haya bila shaka yatakuwa maandalizi bora ya Leopards U-20 kwa Michezo ya awamu ya tisa ya Francophonie ambayo itafanyika nchini DRC hivi karibuni. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.