Pata taarifa kuu

CECAFA: Somalia na Sudan Kusini mabalozi wa Afrika Mashariki kwa wachezaji wasiozidi miaka 17

Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati,  katika mchezo wa soka wa CECAFA, utawakilishwa na Somalia na Sudan Kusini kwenye michuano ya bara Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17, itakayofanyika mwaka ujao nchini  Algeria.

Hamis Kiiza mchezaji wa Uganda Cranes alikuruka kwanja la mchezaji wa Ethiopia kwenye mchezo wa robo fainali michuano ya CECAFA siku ya jumanne
Hamis Kiiza mchezaji wa Uganda Cranes alikuruka kwanja la mchezaji wa Ethiopia kwenye mchezo wa robo fainali michuano ya CECAFA siku ya jumanne RFI
Matangazo ya kibiashara

Somalia ilijikatia tiketi katika mechi yake ya mwihso ya kufuzu baada ya kuishinda Uganda mabao 8-7 kupitia mikwajo ya penalati, katika mechi iliyopigwa jana katika uwanja wa Abebe Bikila jijini Addis Ababa. 

Hali kama hiyo ilikuwa kwa upande wa Sudan Kusini ambayo iliwahsinda Tanzania mabao 4-3 baada ya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya bao moja kwa moja. 

Mbali na kufuzu katika michuano hiyo, Sudan Kusini na Somalia zitamenyana siku ya Jumamosi, kumpata bingwa wa eneo la Afrika Mashaeriki na Kati. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.