Soka: Tanzania yafuzu katika mashindano ya kombe la dunia kwa watu wenye ulemavu
Timu ya Taifa ya Watu wenye ulemavu Tanzania (Tembo Warriors) imefuzu kuingia katika hatua 16 bora katika mashindano ya kombe la dunia la mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Tanzania ilipata ushindi wake wa kwanza wakiifunga Uzbekistan mabao 2-0 huko Uturuki yanapofanyika mashindano hayo.
Tembo Warriors sasa watakutana na Japan katika mchezo ujao.
Tanzania ilikua kundi E pamoja na Spain, Poland na Uzbekistan
Nchi nyingine zilizofuzu katika nafasi hiyo kutoka Afrika ni Morroco na Angola.
Mashindano haya yameandaliwa na Shirikisho la Soka la Asia Magharibi-WAFF na yanafanyika Istanbul, Uturuki hadi 9 Oktoba 2022.