Pata taarifa kuu

Algeria yataka kuwa mwenyeji wa AFCON 2025 badala ya Guinea

Algeria itawania kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mnamo 2025 badala ya Guinea, ametangaza rais wa Shirikisho la Soka la Algeria (FAF), Zefizef Djahid.

Rachid Ghezzal (kushoto) na Ryad Mahrez wakati wa mechi dhidi ya Tunisia.
Rachid Ghezzal (kushoto) na Ryad Mahrez wakati wa mechi dhidi ya Tunisia. RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) lilitangaza Ijumaa kwamba lilikataa michuano ya AFCON ya mwaka 2025 kuchezwa nchini Guinea, ambayo haiko tayari kwa michuano hiyo.

"Algeria itakuwa mwenyeji wa CAN 2025", alitangaza Bw. Djahid siku ya Jumamosi, ambaye alikuwa akizungumza wakati wa droo ya Jumamosi ya michuano ya saba ya mataifa ya Afrika huko Algiers.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hafla hiyo, Patrice Motsepe, rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), alibaini kuwa "nchi kadhaa" zina nia ya kuchukua nafasi ya Guinea.

“Niwahakikishie kuwa hatutachagua nchi ambayo haiko katika kiwango kinachotakiwa kukidhi vigezo vyetu,” alisema bila hata hivyo kutaja nchi hizo.

Morocco, Nigeria na Senegal pia zinaweza kuwa sehemu ya orodha hii.

Siku ya Jumamosi CAF ilikutana na kamati yake ya utendaji mjini Algiers, ambayo ilianza kupokea maombi mapya ya AFCON-2025. Afisa wa shirikisho la Morocco alisema Jumamosi kwamba nchi yake "inafikiria" kuwa mgombea.

"Hakuna nchi itakayopendelewa" kuandaa michuano ya AFCON, hata hivyo, alisema Bw. Motsepe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.