Pata taarifa kuu
RIADHA-KENYA

Mwanariadha wa Kenya, Kibiwott Kandie, avunja rekodi ya mbizo za nusu marathon

Mwanariadha wa Kenya, Kibiwott Kandie, amefanikiwa kuweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za nusu Marathon, baada ya kushinda katika mbio za Valencia. 

Mwanariadha mashuhuri wa Kenya, Eliud Kipchoge, amekuwa mvuto kwa wanariadha wengine kutengeneza rekodi za dunia
Mwanariadha mashuhuri wa Kenya, Eliud Kipchoge, amekuwa mvuto kwa wanariadha wengine kutengeneza rekodi za dunia REUTERS/Athit Perawongmetha
Matangazo ya kibiashara

Kandie alishinda kwa sekunde 29 zaidi ya zile zilizowekwa na Mkenya mwenzake, Geoffrey Kwamworor, katika mbio za Copenhagen mwaka uliopita, akimaliza maili 13.1 katika muda wa dakika 57 na sekunde 32.

Mwanariadha huyu mwenye umri wa miaka 24, alishinda kwa sekunde tano zaidi dhidi ya mwanariadha wa Uganda, Jacob Kiplimo.

Rhonex Kipruto, alimaliza watatu mbele ya Mkenya mwenzake Alexander Mutiso, huku wakimbiaji wote waliomaliza katika nafasi nne za juu wakimaliza ndani ya luda wa rekodi zilizopita.

Katika mbio za wanawake, Muethiopia, Genzebe Dibaba, alishinda kwa sekunde 21 kwa muda wa saa 1 na sekunde 5, huku Mkenya mwingine Sheila Chepkrui akimaliza wapili na Muethiopia, Senbere Teferi, akimaliza watatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.