Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO

Luka Modric ashinda tuzo ya mwaka 2018 ya Ballon d’Or

Luka Modric, kiungo wa kati wa kabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Croatia, ndio mshindi wa tuzo ya mwaka 2018 ya Ballon d’Or. Modric, mwenye umri wa miaka 33, amevunja rekodi ya zaidi ya miaka 10, ambayo imekuwa ikitawaliwa na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Luka Modric wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya AS Roma tarehe 19 Septemba 2018.
Luka Modric wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya AS Roma tarehe 19 Septemba 2018. GABRIEL BOUYS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo, amepata tuzo hiyo, baada ya kuisadia klabu yake kunyakua ligi kuu ya soka nchini Uhispania mara tatu mfululizo.

Aidha, alikuwa wa msaada mkubwa, alipoisadia timu yake ya taifa kufika fainali ya kombe la dunia, licha ya kufungwa na Ufaransa mabao 4-2 mwezi Julai huko nchini Urusi.

"Najiskia vema sana. Nimefurahi sana. Nina hisia nyingi sana wakati huu, sina maneno ya kusema,” alisema Modric baada ya kutajwa mshindi, Jumatatu usiku.

Tuzo la Ballon d'Or ilianza kutolewa mwaka 1956, lakini ilianza kushirikiana na FIFA kati ya mwaka 2010 hadi 2015.

Waandaji wa tuzo hii ni Gazeti la Ufaransa la soka la, France Football.

Cristiano Ronaldo ameshinda taji hili mara tano, mwaka 2008, 2013, 2014, 2016 na 2017 huku Lionel Messi pia akishinda mara tano mwaka 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.