TENISI-WEMBLEDON
Nadal, Federal watinga robo fainali michuano ya Wembledon
Rafael Nadal, mchezaji wa tenisi kutoka Hispania amefuzu moja kwa moja kucheza robo fainali ya michuano ya tenisi ya Wembledon.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Nadal ambaye ni mchezaji namba moja wa tenisi duniani, amemshinda ras wa Jamhuri ya Czech, Jiri Vesely kwa seti 6-3,6-3 na 6-4.
Nadal sasa atachuana na ama Muargentina Juan Martin del Porto au Mfaransa Gilles Simon.
Bingwa mtetezi wa taji hilo, Roger Federal amemshinda Adrian Mannarino kwa seti 6-0, 7-5 na 6-4 dhidi ya Adriano anayeshika nafasi ya 22 kwa ubora duniani.
Federal sasa atachuana na raia wa Afrika Kusini, Kelvin Anderson siku ya Jumatano.