Pata taarifa kuu
SOKA-RAYON SPORTS-RWANDA

Rayon Sports kumtangaza Mbrazil, kuwa kocha wake mkuu

Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda wakati wowote kutoka sasa itamtangaza Mbrazil Roberto Luiz Bianchi kuwa kocha mkuu akichukua nafasi ya Ivan Minneart ambaye ameshushwa kwenye timu ya vijana.

Roberto Luiz Bianchi, Mbrazil anayetarajiwa kupewa kazi ya ukocha na klabu ya Rayon Sports
Roberto Luiz Bianchi, Mbrazil anayetarajiwa kupewa kazi ya ukocha na klabu ya Rayon Sports KT Press
Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka nchini Rwanda zinasema, Bianchi anawasili jioni hii katika Uwanaj wa ndege wa Kigali.

Bianchi ana uzoefu na soka la Afrika ambapo aliwahi kuifundisha Petro Atletico ya Angola na pia aliwahi kuifunza timu ya Taifa ya Angola, Parancras Negros.

Gazeti la New Times la Rwanda, limearifu kuwa Rayon Sports pia imemfuta kazi aliyekuwa kocha mdsaidizi Erick Ndayishimiye.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.