Pata taarifa kuu
CAF-SOKA

CAF yatoa droo ya michuano ya taji la klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza droo ya michuano ya klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.

Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF
Nembo ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF cafoline
Matangazo ya kibiashara

Michuano hii itachezwa nyumbani na ugenini kati ya mwezi Februari na Machi mwaka ujao.

Hii ndio ratiba ya michuano ya hatua ya awali.

Droo ya hatua ya awali taji la klabu bingwa barani Afrika:- 

  • KCCA (Uganda) vs 1 de Agosto (Angola)
  • CF Mounana ( Gabon) vs Vital'O (Burundi)
  • Zanaco (Zambia) vs APR (Rwanda)
  • Ngaya Club (Comoros) vs Yanga Africans (Tanzania)
  • Zimamoto (Zanzibar) vs Ferroviario Beira (Msumbiji)
  • Royal Leopards (Swaziland ) vs AS Vita Club (DRC)
  • Coton Sport (Cameroon) vs Atlabara (Sudan Kusini)
  • AC Leopards (Congo) vs UMS de Loum (Cameroon)
  • Tusker FC (Kenya) vs AS Port-Louis 2000 (Mauritius)

Al-Hilal ya Sudan, TP Mazembe ya DRC, Al-Ahly ya Misri, Zamalek pia ya Misri, Wydad Casablanca ya Morocco, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kuisni, Esperance de Tunis na Etoile du Sahel zote za Tunisia na USM Alger ya Algeria.

Droo ya hatua ya awali taji la  Shirikisho:-

  • Akanda ( Gabon) vs Renaissance du Congo (DRC)
  • Vipers (Uganda) vs Volcan Club (Comoros)
  • KVZ (Zanzibar) vs Le Messager Ngozi (Burundi)
  • Wau Salaam (Sudan Kusini) vs Rayon Sport (Rwanda)
  • Al-Hilal Benghazi (Libya) vs Ulinzi Stars (Kenya)

Azam FC ya Tanzania, ZESCO United ya Zambia, Al-Ahly Shendi ya Sudan na SM Sanga Balende ya DRC zimefuzu katika mzunguko wa kwanza wa michuano hii.

Michuano ya hatua ya makundi itachezwa kati ya mwezi Mei na Julai mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.