Pata taarifa kuu
AFCON 2017

Soka: nchi 16 zilizofuzu kwa AFCON 2017 zajulikana

Mechi za kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) zilimalizika Jumapili Septemba 4, 2016 kwa ushindi wa Burkina Faso, Uganda, DR Congo, Togo na Tunisia. Benin na Jamhuri ya Afrika ya Kati hawamo katika orodha ya timu kumi na sita zitakazoshiriki michuano hiyo nchini Gabon kuanzia Januari 14 hadi Februari 5, 2017.

Mchezaji wa Cote d'Ivoire, Jonathan Kodjia, wakati mechi ya kufuzu katika michuano ya AFCON 2017.
Mchezaji wa Cote d'Ivoire, Jonathan Kodjia, wakati mechi ya kufuzu katika michuano ya AFCON 2017. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya miezi kumi na tano ya hatua hii ya fainali ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, hatimaye timu kumi na sita zitakazoshiriki michuano hiyo zimejulikana. Timu hizi ni Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Cote d'Ivoire, Misri, Gabon, Ghana, Guinea Bissau, Mali, Morocco, Uganda, DR Congo, Senegal, Togo, Tunisia na Zimbabwe.

Kulikuwa na na nafasi tano kwa AFCON 2017, kabla ya mechi za Jumapili Septemba 4, 2016. Nafasi bizi zimechukuliwa kwanza na Burkina Faso pamoja na Uganda. Timu ya taifa ya Burkina Faso ilimaliza ikiwa ya kwanza katika Kundi D, kwa ushindi dhidi ya Botswanaya mabao 2-1. Uganda wamechukua nafasi ya pili, ikikiwa naalama 13.

Togo yafuzu badala ya Benin katika michuano ya AFCON 2017

Benin na ilikua na matumaini ya kuchukua kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2017. Lakini ndoto zao ziligonga mwamba, na kujikuta nafasi yao inachukuliwa na Mali katika kundi C. Benin waliburuzwa na Mali kwa mabao 5-2 mjini Bamako. Mali hata hivyo ilikua na uhakika wa kucheza michuano ya AFCON2017.

Hatimaye Togo ilichukua nafasi ya mwisho ya fainali ya michuano hii. Togo walimaliza wakiwa wa pili katika Kundi A nyuma ya Tunisia, kufuatia wa mabao 5-0 dhidi ya Djibouti na Tunisia waliwabwagiza Liberia kwa mabao 4-1.

Ushindi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ulikua umetabirika Chui wa DR COngo walipata ushindi mkubwa wa mabao 4-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mjini Kinshasa. Timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Fauves Bas-Oubangui, hawatashiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Jamhuri ya Afrika ya kati walimaliza wakiwa pili katika Kundi B nyuma ya Congo-Brazzaville.

Nigeria kutoshiriki AFCON 2017

Timu moja kubwa katika ulimwengu wa soka barani Afrika, Nigeria, haitoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Nigeria ilimaliza ya pili katika Kundi G nyuma Misri. Hiyo itakuwa fursa kubwa kwa Misri kurudi kushiriki michuano hii baada ya miaka saba ya kutokuwepo katika micuano hii.

Cote d'Ivoire, wanaoshikilia taji la ubingwa katika michuano hii, pia wamejikatia tiketi ya kushiriki kwa mara nyingine michuano hii itakayochezwa nchini Gabon.

Jumla ya timu kumi zilishiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 nchini Equatorial Guinea. Guinea-Bissau, watashiriki kwa mara ya kwanza katika michuano hii ya kifahari barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.