Soka-OM: Abou Diaby kushiriki mchuano dhidi ya Gérone
Abou Diaby hatimaye atakua katika kikosi cha wachezaji kumi na moja cha OM ambacho kinachuana Jumatano hii usiku dhidi ya Gérone mechi yao ya kirafiki. OM watakua ugenini.
Imechapishwa:
Abou Diaby, ambaye hajacheza mchezo wa maandalizi kutokana na jeraha la kifundo cha mguu wake wa kushoto alilolipata mwishoni mwa msimu uliopita, atakuwa miongoni mwa wachezaji kumi na mmoja watakao anza mechi hii.
Kocha wa OM Franck Passi, anasema ana imani kwamba Abou Diaby ataonyesha umaarufu wake, baada ya kupona jeraha alilokua akiuguza
Kikosi cha OM kinaundwa na Pelé, Sakai, Hubocan, Doria, Bedimo, Diaby, Machach, Alessandrini (katikati), Cabella, Khaoui, Gomis