Pata taarifa kuu
CLAUDE LEROY-TOGO

Togo yasema haitamfuta kazi kocha wake mkuu wa timu ya taifa

Shirikisho la soka nchini Togo, linasema kuwa halitamfuta kazi kocha wake mkuu wa timu ya taifa, Mfaransa, Claude LeRoy, licha ya waendesha mashtaka nchini Ufaransa kutaka ahukumiwe kifungo jela.

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Racing ya Ufaransa, Claude LeRoy na Patrick Proisy
Aliyekuwa kocha wa klabu ya Racing ya Ufaransa, Claude LeRoy na Patrick Proisy DR
Matangazo ya kibiashara

LeRoy, anakabiliwa na kesi kuhusu ushiriki wake wa uuzaji wa wachezaji katika klabu ya Racing makosa anayodaiwa kuyatenda kati ya mwaka 1990 na 2000.

Waendesha mashtaka wa mahakama kuu mjini Strasbourg, juma lililopita waliiomba mahakama imuhukumu kifungo cha miaka cha miwili jela, huku kifungo cha miezi kumi na nane wakitaka kiahirishwe kwa muda.

LeRoyo mwenyewe akihojiwa hivi karibuni, alisema kuwa anafahamu sakata la uuzwaji wa wachezaji hao, na kwamba binafsi anaamini hakufanya kosa lolote na nimsafi.

Kwa sasa kocha huyo anasubiri uamuzi wa rais wa mahakama kuu ya Strasbourg, anaotarajiwa kuutoa September 13 mwaka huu.

Mbali na kocha huyo, waendesha mashtaka pia wanataka aliyekuwa rais wa klabu hiyo, Patrick Proisy kuhukumiwa kifungo cha miaka 3 jela.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa kulikuwa na nyaraka nyingi za kughushiwa za kampuni ya uwaka wa wachezaji IMG, sambamba na makampuni mengine ambayo yalinufaika kwa kukwepa kulipa kodi kutokana na uhamisho mbalimbali wa wachezaji.

LeRoy amekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Togo toka mwezi Aprik mwaka huu, alipochukua nafasi ya Tom Saintfiet.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.