Pata taarifa kuu
UGANDA-SOKA

Lweza FC yaimenya Saints FC 2-0

Klabu ya soka ya Lweza FC nchini Uganda iliilemea Saints FC mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa ligi kuu ya soka nchini humo.

Kikosi cha wachezaji kumi na moja cha timu ya taifa ya Uganda katika mechi ya kwanza ya kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Burkina Faso, Machi 26, 2016.
Kikosi cha wachezaji kumi na moja cha timu ya taifa ya Uganda katika mechi ya kwanza ya kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Burkina Faso, Machi 26, 2016. AHMED OUOBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mchuano huo ulichezwa Jumanne jioni katika uwanja wa Mutesa II katika eneo la Wankulukuku jijini Kampala.

Mabao yote ya Lweza FC yalitiwa kimyani na Juma Balinya na Geoffrey Sserunkuma katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Vijana wa Lweza FC walionekana bora katika mchuano huo huku wachezaji Paddy Muhumuza na Emmanuel Kalyowa wakitawala safu ya mchuano huo.

Ushindi huu, umewafikisha Lweza FC katika nafasi ya 9 ikiwa na alama 30 huku Saints FC ikisalia katika nafasi ya 13 kwa alama 19 baada ya michuano 20 kuchezwa.

Wachezaji:

Lweza FC: Charles Lukwago (G.K), Fred Okot, Nestroy Kizito, Michael Kabanda, Ibrahim Kiyemba, Ayub Kisaliita, Paddy Muhumuza, Moses Ndawula (81'Mustapha Kiragga ), Geofrey Sserunkuma (71' Rajab Kakooza), Sula Bagala, Juma Balinya (75' John Kisakye).

Saints F.C : Yasin Mugabi (G.K), Fred Agandu, Hassan Musana, Marlon Tangawuzi, Bernard Agele, Fahad Kawooya, Ivan Kiweewa (57'Eric Sebuguzi, ), Isaac Kirabira, Yasin Mugume, Patrick Senfuka (39' George Ssenkaaba), Alex Kitata (70' Nicolas Odong).

Matokeo Kamili:-

Bright Stars FC 1-2 KCCA FC

BUL FC 2-0 Express FC

Lweza FC 2-0 The Saints FC

Maroons FC 1-1 JMC Hippos FC

SC VU 0-3 Sadolin Paints FC

URA FC 3-2 Simba FC

Police FC 0-0 Vipers SC

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.