Pata taarifa kuu
CHAN-RWANDA

Mali yatinga fainali michuano ya CHAN, sasa kucheza na DR Congo siku ya Jumapili

Timu ya taifa ya Mali imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani barani Afrika, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ivory Coast.

Mchezaji wa Mali mwenye jezi ya njano akipiga mpira mbele ya mchezaji wa Ivory, wakati timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa nusu fainali mjini Kigali
Mchezaji wa Mali mwenye jezi ya njano akipiga mpira mbele ya mchezaji wa Ivory, wakati timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa nusu fainali mjini Kigali RFI
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji wa Mali aliyeingia kipindi cha pili, Yves Bissouma aliifungia bao timu yake kwenye dakika ya 89 ya mchezo, na kuipeleka timu yake hatua ya fainali na sasa itacheza na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, siku ya Jumapili.

Mechi ya mshindi wa tatu wa michuano ya mwaka huu inatarajiwa kupigwa siku hiyohiyo ya Jumapili, ambapo timu ya taifa ya Guinea itapepetana na Ivory Coast.

Katika mchezo huo timu ya Mali inabidi ijilaumu yenyewe kwakuwa kwenye dakika ya 32 ya mchezo kipindi cha kwanza ilipata nafasi ambayo ingewafanya waongoze, baada ya timu hiyo kuzawadia penalty na mwamuzi, lakini mchezaji, Mamadou Coulibaly alikosa penalty yake baada ya kupanguliwa na mlinda mlango wa Ivory Coast Ali Sangare Badra.

Kipa wa Mali Djigui Diarra.
Kipa wa Mali Djigui Diarra. AFP PHOTO / MARTY MELVILLE

Mali maarufu kama The Eagles nao waliponea chupuchupu baada ya mchezaji wa Ivory Coast, Essis Aka kuachia fataki akiwa umbali mrefu na shuti lake kugonga mwamba wa juu.

Marabaada ya kukoswakoswa, timu ya Mali ililazimika kufanya mabadiliko na kumuingiza Kouame N'Guessan mapema kabisa katika kipindi cha pili akichukua nafasi ya Coulibaly, nafasi ambayo mshambuliaji huyo aliitumia ipasavyo.

Bao la dakika za lala salama lililofungwa na Bissoumas limeipeleka timu ya taifa ya Malia kwenye fainali yake ya kwanza ya michuano hii mikubwa barani Afrika ambapo sasa itacheza na DR Congo siku ya Jumapili.

DR Congo ni mabingwa wa michuano hii wakati ilipoanzishwa mwaka 2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.