Pata taarifa kuu
DAKAR 2016-MASHINDANO

Dakar: mbio kwa pikipiki kukatishwa, kufupishwa kwa magari

Hatua ya 9 ya mashindano ya mbio ya magari na pikipiki (Dakar-2016) imekatishwa kwa pikipiki na kufupishwa kwa magari, kwa sababu ya joto kali na matatizo mengi ya uendeshaji wanayokumbana nayo washindani, wandaaji wamesema Jumanne hii.

Gari la raia wa Qatar Nasser Al-Attiyah katika hatua 9 ya mashindano ya mbio ya magari (Dakar 2016), Januari 12, 2016 katika mji wa Belen.
Gari la raia wa Qatar Nasser Al-Attiyah katika hatua 9 ya mashindano ya mbio ya magari (Dakar 2016), Januari 12, 2016 katika mji wa Belen. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa pikipiki, mbio zimekatishwa kwenye umbali wa kilomita 179 ya siku maalum. Jumla ya waendesha pikipiki watajiunga na msafara unaotokea katika mji wa Fiambala, ispokuwa pikipiki zaidi ya thelathini ambazo zimevuka daraja ambalo ni hatari, na linaweza kusababisha ajili, wandaaji hao wameongeza.

Kwa magari, siku maalum imefupishwa na yatalazimika kufanya umbali wa kilomita 179.

Pikipiki zitalazimika kutembea kwenye umbali wa kilomita 436 kati ya mji wa Belen na mji wa Fiambala, na magari yatafanya umbali wa kilomita 396, ikiwa ni pamoja na 285 yanayoshindana kwa makundi yote mawili kwa wakati muafaka.

Joto kati ya nyuzi 37 na 40 zimehifadhiwa kwenye kifungu cha wakati muafaka.

Baada ya kuwasili kwa pikipiki katika siku maalum, raia wa Australia, Toby Price (KTM), anayeongoza katika mashindao ya ujumla, ameendesha pikipiki yake kwa muda mzuri wa saa 3, dakika 55 na sekunde 51. Lakini waandaaji wanaweza kuamua kuacha kuhesabu muda ili kusimamia kwa kilometa 179, ambapo Price pia anaongoza kwa muda mzuri wa kasi. Muda wowote utatolewa kwa waendesha piki piki ambao hawafikia hatua hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.