Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-MCHEZAJI BORA

Mchezaji bora wa soka duniani kutunzwa Jumatatu

Leo Jumatatu, kutakuwa na hafla ya kumtuza mchezaji bora wa mchezo wa soka duniani alimaarufu kama FIFA Ballon d'or kwa mwaka wa 2015.

Jumatatu hii Januari 11, 2016, katika makao makuu ya FIFa kutakua na hafla ya kumtunza mchezaji bora wa soka duniani mwaka 2015.
Jumatatu hii Januari 11, 2016, katika makao makuu ya FIFa kutakua na hafla ya kumtunza mchezaji bora wa soka duniani mwaka 2015. REUTERS/Ruben Sprich/Files
Matangazo ya kibiashara

Hafla hiyo itafanyika jijini Zurich nchini Uswizi, jiji ambalo pia ni Makao makuu ya Shirikisho la soka duniani FIFA.

Wachezaji watatu wanaowania taji hilo ni Lionel Messi raia wa Argentina anayeichezea klabu ya Barcelona nchini Uhispania pamoja na mchezaji mwezake Neymar ambaye anatokea nchini Brazil. Lakini mshindi wa mwaka 2014 Christian Ronaldo raia wa Ureno pia anatetea taji hili.

Lionel Messi ameshinda taji hili mara nne mfululizo mwaka 2009, 2010, 2011 na 2012 na anasaka taji la tano.

Christiano Ronaldo naye ameshinda mara mbili mfululizo mwaka 2013 na 2014 na pia aliwahi kushinda mwaka 2008 naye anatafuta taji la ne.

Msimu uliopita, Messi aliifungia klabu yake mabao 58, na kuisadia klabu yake kunyakua ubingwa wa klabu bora duniani michuano iliyofanyika mwezi Desemba mwaka jana nchini Japan.

Ronaldo akitikisa nyavu mara 61 na Neymar akifunga mabao 39.

Wanaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka ni Luis Enrique raia wa Uhispania ambaye ni kocha wa Barcelona, Pep Guardiola pia raia wa Uhispania na kocha wa Bayern Munich nchini Ujerumani. Kocha mwingine ni Jorge Sampaoli raia wa Argentina kocha wa timu ya taifa ya Chile aliisadia kunyakua taji la Copa America.

Wanaowania taji la mwanadada au mwanamke bora katika mchezo huu wa soka ni pamoja na mchezaji wa timu ya taifa ya Marekani na klabu ya Houston Dash, Celic Sasic kutoka Ujerumani na Aya Miyama kutoka Japan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.