Pata taarifa kuu
SOKA-DAKAR-CAF

Michuano inayowashirikisha vijana wasiozidi miaka 20 yaanza Dakar

Michuano ya soka kuwania ubingwa wa bara la Afrika baina ya wachezaji wasiozidi miaka 20 inaanza leo jijini Dakar nchini Senegal.

Mji mkuu wa Senegal, Dakar, ambao unasubiri kupokea timu mbalimbali zitakazoshiriki michuano ya soka kuwania ubingwa wa bara la Afrika baina ya wachezaji wasiozidi miaka 20.
Mji mkuu wa Senegal, Dakar, ambao unasubiri kupokea timu mbalimbali zitakazoshiriki michuano ya soka kuwania ubingwa wa bara la Afrika baina ya wachezaji wasiozidi miaka 20. Wikimedia Commons/Initsogan
Matangazo ya kibiashara

Haya ni Makala ya 20, na Mataifa manane yanashiriki.

Mataifa hayo ni pamoja na wenyeji Senegal, Congo Brazavile, Ghana, Cote d'Ivoire, Mali, Nigeria, Afrika Kusini na Zambia.

Timu zipo katika makundi mawili, kundi la A kuna wenyeji Senegal, Nigeria, Congo Brazaville na Ivory coast au cote d'Ivoire.

Kundi B kuna Ghana, Afrika Kusini, Mali na Zambia. Mabingwa watetezi Misri hawakufuzu katika michuano ya mwaka huu.

Mchuano wa ufunguzi ni kati ya wenyeji Senegal na Nigeria kuanzia saa moja na nusu jioni saa za Afrika Mashariki sawa na saa kumi na mbili na nusu saa za Afrika ya Mashariki, na mchuano wa pili ni kati ya Congo Brazaville na Cote d'Ivoire saa nne na nusu usiku saa za Afrika Mashariki Sawa na saatatu usiku saa za Afrika ya Kati.

Jumatatu Machi 9, mechi za kundi B zitapigwa na mchuano wa kwanza utakuwa kati ya Ghana na Afrika Kusini, na baadaye Mali na Zambia.

Mechi ya fainali itakuwa tarehe 22 mwezi huu lakini mataifa manne yatakayofika katika hatua ya nusu fainali watafuzu katika michuano ya kombe la dunia nchini New Zealand kati ya tarehe 30 mwezi Mei hadi tarehe 20 mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.