Pata taarifa kuu
Football

Nicolas Anelka asaini mkataba na klabu ya Atletico Mineiro ya Brazil

Baada ya kuondoka katika Klabu ya ligi kuu nchini Uingereza ya West Bromwich Albion March 14 iliopita, mshambuliaji wa Kimataifa wa Ufaransa Nicolas Anelka amesaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Atletico Mineiro ya nchini Brazil. Taarifa hizi zimetolewa na rais wa klabu hiyo Alexandre Kalil.

Nicolas Anelka asaini na klabu ya brazil Atletico Mineiro
Nicolas Anelka asaini na klabu ya brazil Atletico Mineiro REUTERS/Darren Staples
Matangazo ya kibiashara

Nicolas Anelka mchezaji mwenye utata wa mara kwa mara, atakuwa amesajiliwa kwa mara ya kumi na mbili kuvichezea vilabu tofauti.

Anelka mwenye umri wa miaka 35 amevichezea vilabu kadhaa vikiwemo Paris Saint Germain, Arsenal, Real Madrid na Chelsea. Klabu ya mwisho kuichezea na mchezaji huyo wa kimataifa wa nchini Ufaransa ilikuwa ni klabu ya West Bromwich Albion, ambayo ilikuwa na mpango wa kumtimuwa kutokana na ishara ya ubaguzi wa kiyahudi alionyesha mwezi Desemba iliopita.

Ligi kuu nchini Uingereza ilitowa adhabu kwa mchezaji huyo wa kimataifa kwa kumfungia kucheza mechi tano za kimataifa na kutowa faini ya pauni elfu thamanini, sawa na Euro elfu tisini na saba baada ya kuonyesha ishara hiyo ambayo yeye ameendelea kukanusha kuwa haina uhusiano wowote na ishara ya ubaguzi wa wayahudi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.