Pata taarifa kuu
Brazili

Ujenzi wa uwanja wa mpira mjini Amazonia ambao utapokea michuano ya kombe la dunia umesitishwa na vyombo vya sheria

Shuguli za ujenzi wa uwanja wa mpira wa Manaus, mjini Amazonia, zimesimamishwa na vyombo vya sheria vya Brazili. Katika taarifa iliotolewa jana jumapili, ofisi ya muendesha mashitaka mjni Amazonia imesitisha mara moja shughuli hio. Uamzi huo umechukuliwa kufuatia vifo vya wafanyakazi wawili kwenye uwanja huo ambao utapokea mechi za kombe la dunia mwezi wa juni mwakani.

Uwanja wa soka wa Manaus mjini Amazonia
Uwanja wa soka wa Manaus mjini Amazonia REUTERS/Gary Hershorn/Files
Matangazo ya kibiashara

Wakaguzi na waendesha mashitaka wanasubiriwa kwenye uwanja huo. Usalama wa wafanyakazi umezingatiwa, hasa wale ambao watahusika na kutia paa kwenye urefu wa takribani kilomita 10.
Ofisi ya mashitaka imefahamisha kwamba hatua iliochukuliwa haitorejelewa iwapo Shirika linalojihusisha na ujenzi wa uwanja huo litawahakikishia kuweka mazingira bora ya kazi kwa wafanyakazi wake.
Vifo vya wafanayakazi hao vimetokea baada ya ajali nyingine iliosababisha vifo vya watu wawili kweny uwanja wa São Paulo ambao utapokea sherehe za uzinduzi wa kombe la dunia la mpira wa miguu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.