Pata taarifa kuu
SOKA

Zambia, Malawi na Cote Dvoire waalikwa michuano ya CECAFA

Baraza la soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA limetangaza kupitia tovuti yake kuwa limezialika timu za Malawi, Zambia na Cote Dvoire kushiriki katika makala ya mwaka huu ya taji hilo kama wageni litakalofanyika jijini Nairobi nchini Kenya kati ya tarehe 27 na 12 mwezi Desemba mwaka huu.

Cecafa
Matangazo ya kibiashara

CECAFA inasema kuwa michuano hiyo imeratibiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya soka katika miji ya Nairobi, Kisumu, Mumias, Nakuru na Mombasa.

Kamati andalizi ya michuano hiyo ilikutana jijini Nairobi siku ya Jumanne chini ya Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye na rais wa chama cha soka nchini humo Sam Nyamweya kuweka mikakati ya kufanikisha michuano hiyo ikiwemo mipangilio ya usalama na sehemu watakazoishi wachezaji.

Michuano ya CECAFA mwaka huu inafanyika nchini Kenya kipindi hiki nchi hiyo ikiadhimisha miaka 50 ya Uhuru waka tarehe 12 mwezi Desemba siku ambayo pia mchuano wa fainali utachezwa katika uwanja wa taifa wa Nyayo jijini Nairobi.

Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF Issa Hayatou amekubali ombi la chama cha soka nchini Kenya kuwa mgeni rasmi wakati wa michuano hiyo baada ya kufanya hivyo nchini Uganda mwaka uliopita.

FKF inaahidi michuano ya kipekee baada ya makala ya mwaka jana kufanyika jijini Kampala nchini Uganda na wenyeji Uganda Cranes kuibuka mabingwa kwa kuwafunga Kenya katika uwanja wao wa nyumbani wa Namboole.

Mbali na mataifa yaliyoalikwa katika michuano hiyo, mataifa wanachama wa CECAFA yatakayoshiriki ni pamoja na wenyeji Kenya, mabingwa watetezi Uganda, Tanzania, Rwanda, Sudan, Burundi, South Sudan, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Zanzibar na Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.