Pata taarifa kuu
GOLF

Mshindi wa Mashindano ya Golf ya Muirfield Phil Mickelson amekiri hakutarajia kama angeibuka kinara wa Taji hilo

Mchezaji wa Golf kutoka nchini Marekani Phil Mickelson aliyeibuka mshindi wa mashindano ya Muirfield amekiri ushindi wake ni sehemu ya harakati zake za maisha kwani hakutegemea kama angeibuka na taji hilo.

Mshindi wa Taji la Muirfield kwenye Golf Phil Mickelson akiwa ameshikilia Taji lake
Mshindi wa Taji la Muirfield kwenye Golf Phil Mickelson akiwa ameshikilia Taji lake
Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Mickelson kwenye mzungumko wa 66 ndiyo ulimfanya aibuke mshindi wa kinyang'anyiro hicho ambacho kilikuwa ni kugumu kwa washiriki ambao wote walikuwa wanalimezea mate taji hilo.

Mickelson amekiri ushindi huo utaendelea kusalia kwenye kumbukumbu zake kwa kuwa hakutegemea kama angeweza kuimarisha ubora wa uchezaji wake katika kipindi hifupi na hatimaye kutwaa taji hilo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 43 aliingia kwenye mzunguko wa 66 akiwa amezidiwa mipigo mitano lakini akafanya vizuri na kufanikiwa kushinda kitu kilichosaidia kumpatia taji.

Mickelson alifanikiwa kushinda taji kubwa kwenye mchezo wa golf kwa mara ya kwanza mwaka 2004 lakini baada ya hapo aliweza kupata mafanikio kwa kushika nafasi ya pili mwaka 2006 lakini mara nyingine hakuwa na matokeo mazuri.

Raia huyo wa Marekani ameweka bayana taji hilo la Muirfield litakuwa chachu kwake kuweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine hasa US PGA Tour ambalo amekuwa akiota kulitwaa.

Mickelson amewataka mashabiki wake kuendelea kumuunga mkono kwani anatarajia kufanya mambo makubwa zaidi katika mashindano mengine anayotarajiwa kushiriki na kuwapa wakati mgumu vigogo kwenye mchezo wa Golf duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.