Pata taarifa kuu
Ghana

Ufaransa kumenyana na Uruguay Fainali za kombe la dunia kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 20

Ufaransa itamenyana na Uruguay katika fainali ya kombe la dunia ya mchezo wa soka baina ya wachezaji wasiozidi miaka 20 siku ya Jumamosi baada ya kufika fainali Jumatano usiku nchini Uturuki. 

Wachezaji wa Soka wa Ghana walio na Umri usiozidi miaka 20
Wachezaji wa Soka wa Ghana walio na Umri usiozidi miaka 20
Matangazo ya kibiashara

Vijana wa Ghana ambao walikuwa wamepewa nafasi kubway a kunyakua taji hili walifungwa na Ufaransa mabao 2 kwa 1.

Mfaransa Florian Thauvin ndiye aliyeifungia timu yake mabao yote mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili.

Bao la pekee la Ghana lilitiwa kimiani na Ebenezer Assifuah, na kusawazisha kabla ya Ufaransa waliokuwa na wachezaji kumi uwanjani baada ya mchezaji wake Samuel Umtiti kuoneshwa kadi nyekundu na atakosa mchezo wa fainali.

Ghana ilikuwa taifa la kwanza la Afrika kushinda taji hilo la dunia mwaka 2009 baada ya kuwafunga Brazil mwaka 2009 kupitia mikwaju ya Penati.

Uruguay nao walifika fainali baada ya kuwashinda mabao 7-6 Iraq kupitia mikwaju ya penati baada ya timu zote mbili kutoka sare ya bao 1 kwa 1 katika muda wa kawaida na ule wa ziada.

Ghana na Iraq watamenyana kutafuta mshindi wa tatu kabla ya mchuano wa fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.