Pata taarifa kuu
Sudani

Michuano ya Cecafa yaanza leo

Michuano ya soka kuwania ubingwa wa klabu bora katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati inafungua milango yake hii leo  katika majimbo ya Darfur na Koridafn Kusini nchini Sudan. 

Matangazo ya kibiashara

Mchuano wa ufunguzi ni kati ya wenyeji Al Shandy FC ya Sudan na klabu ya mapato ya Uganda URA katika uwanja wa Kadguli katika jimbo la Korodofan Kusini .
 

Siku ya Jumatano Elman itachuana na APR ya Rwanda katikam mchuano kwa kwanza huku Merreikh ikimenyana na Vitalo.
 

Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye amesema kuwa michuanon hiyo itaendelea kama ilivypangwa na usalama umeimarishwa katika viwanja vyote na hoteli za wachezaji.
 

Mashindani haya yanaanza bila ya mabingwa watetezi Yanga FC ya Tanzania na klabu nyingne ya Simba FC , Falcon FC ya Zanzibar na Tusker FC ya Kenya kujiondoa kwa sababu za kiusalama lakini serikali ya Tanzania baada ye iliwaruhusu timu zao kusafiri baada ya kuhakikishiwa usalama na serikali ya Sudan.
 

Hata hivyo,Musonye amesema kuwa hatavikubali vlabu hivyo kuhudhuria michuano hiyo na hata wakija watasalia kuwa tu mashabiki kwa kile walichosema wamekubali kutumiwa na maadui wa CECAFA.
 

Nafasi ya vilabu hivyo vilivyojiondoa itachukuliwa na klabu ya mapato ya Uganda URA, Rayon Sport ya Rwanda na Elect Sport ya Chad.
 

Timu zitakazoshiriki katika mashindano hayo ya klabu bingwa katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati yanayafadhiliwa kwa kiasi kikubwa  na rais wa Rwanda Paul Kagame ni pamoja na Al Ahly Shandi (Sudan), Al Nasir (South Sudan), Al-Hilal Kadugli (Sudan), Express FC (Uganda), URA FC (Uganda), Ports FC (Djibouti), Vital'O (Burundi), Merriekh El Fasher (Sudan), APR (Rwanda), Elman (Somalia), Rayon Sport (Rwanda) and Elect Sport (Chad)
.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.