Pata taarifa kuu
SOKA

Wachezaji wawili wa Togo wakataa kusafiri Libya kwa sababu za kiusalama

Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Togo wamejiondoa kwenye kikosi kitakachomenyana na Libya siku ya Ijumaa jijini Tripoli katika mchuano wa kufuzu kwa kombe la dunia nchini Brazil mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Alaixys Romao na mwenzake Jonathan Ayite wamejiondoa kwa kile wanachokisema kuwa wanahofia usalama wao jijini Tripoli kutokana na hofu ya kuzuka kwa makabiliano makali kati ya wandamanaji na makundi ya waasi na kusababisha vifo vya watu 30 mwishoni mwa juma lilillopita.

Romao ni mmoja wa wachezaji walioshuhudia mashambulizi ya wachezaji wenzake na wawili wakapoteza maisha mwaka 2010 wakati walipokuwa wanaelekea nchini Angola kushiriki katika mashindano ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika.

Wachezaji hao wanasema kuwa watakubali kusafiri Libya iwapo tu shirikisho la soka duniani FIFA litawahakikishia usalama wao wakati wa mchuano huo.

Shirikisho la soka la Togo FTF linasema kuwa wachezaji wake wengi ambao wana uraia wa Ufaransa wanahofia usalama wao jijini Tripoli hasa kutokana na serikali ya Ufaransa kuwaonya raia wake kutosafiri nchini Libya kwa sababu za kisaulama.

Ijumaa uiliyopita, timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikuwa timu ya kwanza kucheza jijini Tripoli tangu kumalizika kwa mapigano nchini humo na mchuano kumalizika sare ya kutofungana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.