Pata taarifa kuu
SOKA

Tanzania kumenyana na Sudani Kusini katika mechi ya kirafiki leo jijini Addis Ababa

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars jumapili hii inamenyana na Sudan Kusini katika mechi ya kimataifa ya kirafiki jijini Addis Ababa ikiwa ni mwendelezo wa harakati za Stars kuwania kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014.

www.shaffihdauda.com
Matangazo ya kibiashara

Stars ambao wamepiga kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia wakiwa na mkufunzi wao Kim Paulsen wanatarajia kupata matokeo mazuri katika mechi hiyo inayowaandaa kukabiliana na Morocco jumamosi ijayo mjini Marrakech.

Katika mechi ya kwanza dhidi ya Morocco iliyopigwa jijini Dar es salaam nchini Tanzania mwezi machi, Stars waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Stars kwa sasa ipo katika nafasi ya pili katika Kundi C lenye timu za Ivory Coast, Morocco na Gambia. Ivory Coast inaongoza kundi hilo ikiwa na 7, ikifuatiwa na Tanzania yenye alama 6, Morocco wana alama 2 na Gambia inashika mkia kwa alama 1.

Ili vijana wa Tanzania waweze kufuzu wanatakiwa kushinda kwenye mechi zote tatu ili waongoze kundi C ndipo watapata nafasi ya kuingia timu kumi za Afrika ambazo zitachuana ili kupara timu tano bora zitakazoliwakilisha bara la Afrika nchini Brazil katika fainali za kombe la dunia kwa mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.