Pata taarifa kuu
Michezo

Kocha wa Uganda Cranes kutaja kikosi kipya

Kocha wa timu ya taifa ya Uganda Milutin 'Micho' Sredojevic hatakuwa na muda wa mapumziko wakati huu ambapo anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuandaa kikosi cha taifa kitakachoumana na kikosi cha Libya katika mechi ya kirafiki hivi karibuni.

Martin  Mutumba mshambuliaji wa pembeni anayechezea klabu ya AIK Stockhom ya nchini Sweden amerejea kikosini.
Martin Mutumba mshambuliaji wa pembeni anayechezea klabu ya AIK Stockhom ya nchini Sweden amerejea kikosini. foto.jesperzerman.se
Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo ambaye ana umri wa miaka 43 anambadili Bobbby Williamson kwa kuongezewa mkataba wake kwa miaka miwili baada ya kuondolewa kwa Williamson mwezi uliopita.

Kamati ya ufundi ya shirikisho la kandanda nchini Uganda limetoa kikosi cha wachezaji 37 kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kirafiki baina ya timu yake na Libya mwezi ujao mchuano utakaowapasha misuli kwa ajili ya mechi ya kufuzu kombe la dunia mnamo June 8 itakayopigwa Namboole dhidi ya Liberia.

Kikosi hicho kinajumuisha walinda mlango watano,walinzi kumi na wawili,viungo kumi na wawili na washambuliaji nane.

Mshambuliaji wa pembeni anayecheza AIK Stockhom nchini Sweden Martin Mutumba amerejea kikosini kwa mara ya kwanza tangu kujionyesha kupinga Senegal mwezi june mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.