Pata taarifa kuu
DRCongo - CAF

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaomba kuandaa michuano ya soka ya Afrika mwaka 2019

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema imewasilisha ombi kwa Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuwa mwenyeji wa dimba la mataifa ya Afrika mwaka 2019.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa michezo wa nchi hiyo Baudouin Banza Mukalay Nsungu amesema taifa lake liko tayari kuandaa mashindano hayo makubwa barani Afrika mwaka huo ikiwa watapata nafasi hiyo.

Aidha, Waziri huyo ameongeza kuwa wametoa ombi hilo kwa ushirikiano na shirikisho la soka nchini huo FECOFA na wana matumaini makubwa kuwa watapata nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Mukalay ameongeza kuwa ikiwa DRC itapata nafasi ya kuandaa taji hilo basi litaandaliwa jijini Kinshasa na Lumbumbashi huku akisisitiza kuwa uwanja katika mji wa Mtadi Magharibi mwa nchi hiyo na mwingine mjini Kisangani utakuwa tayari kuandaa michuano hiyo.

Mashindano ya mwaka huu wa 2013 yaliandaliwa nchini Afrika Kusini, huku yale ya mwaka 2015 yakitarajiwa kufanyika nchini Morrocco.

Libya imeorodheshwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo mwaka 2017 baada ya kuyashinda mataifa kama Bostwana, Guinea na Zambia ambayo pia yalikuwa katika harakati za kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.