Pata taarifa kuu
AUSTRALIA OPEN 2013

Azarenka na Li Na watinga fainali upande wa wanawake kwenye michuano ya Australia Open

Michauno ya Australia Open imeendelea kushika kasi nchini humo huku upande wa wanawake ikifikia hatua ya fainali na wanaume ni kucheza nusu fainali.

Roger Federer akifurahi baada ya kushinda mechi yake
Roger Federer akifurahi baada ya kushinda mechi yake REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Katika mechi zilizochezwa siku ya Jumatano, mchezaji Victoria Azarenka alifanikiwa kutinga kwenye hatua ya fainali baada ya kufanikiwa kumfunga msichana kinda anayeibukia kwenye mchezo huo Sloane Stephens.

Azarenka alifanikiwa kutinga hatua ya fainali kwa kumfunga Sloane kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-1 na 6-4 kwenye mchezo ambao Azarenka aliweza kummudu vilivyo mpinzani wake.

Sloane alifanikiwa kufika hatua ya nusu fainali baada ya kumfunga Serena William kwenye mchezo ambao hata hivyo Serena alikuwa na maumivu.

Katika mchezo mwingine mwanadada Li Na alifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kumfunga Maria Sharapova kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-1 na 6-2, kwenye mchezo uliokuwa na upinzani mkali.

Kwa matokeo hayo sasa fainali kwa upande wa wanawake utawakutanisha Li Na na Victoria Azarenka.

Kwa upande wa wanaume Andy Murray ametinga hatua ya nusu fainali baada ya kumfunga Chardy kwa seti tatu bila kwa matokeo ya 6-4. 6-1 na 6-2 wakati Roger Federer akimfunga Joe Tsonga kwa seti tatu bila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.