Pata taarifa kuu
michezo

Novak Djokovic ajiandaa kwa tahadhari kutetea ubingwa wa kombe la Australia Open

Bingwa namba moja duniani katika mchezo wa Tennis Novak Djokovic ameonesha kupata hofu kuhusu iwapo ataweza kutetea ubingwa wake katika michuano ya Australia Open baada ya kushindwa kutamba katika michuano ya fainali za kombe la Hopman jana usiku. 

Novak Djokovic
Novak Djokovic REUTERS/Suzanne Plunkett
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza baada ya yeye na Ana Ivanovic kufungwa na Wahispania Anabel Madina Garrigues na Fernando Verdasco katika makundi ya timu mchanganyiko,Bingwa huyo mtetezi wa kombe la Australia Open tayari amekuwa akiangazia kutetea ubingwa wake.

Wakati huo huo timu za Serbia pia zimeshindwa kuwika kwa karibu mara ya tatu katika michuano hiyo ya kombe la Hopman,Djokovic amehitimisha maandalizi yake ya mwisho kwa ajili ya kombe la Australia Open kwa kumchakaza bingwa namba kumi wa zamani Verdasco katika seti za moja kwa moja 6-3, 7-5.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.