Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Kocha Mkuu wa QPR Redknapp ana matumaini Timu yake haitoshuka daraja licha ya kupata matokeo mabaya

Kocha Mkuu wa Klabu ya Queens Park Rangers Harry Redknapp ameendelea kusisitiza timu hiyo itajiondoa kwenye baa la kushuka daraja licha ya kupata kichapo cha magoli 3-0 mbele ya Liverpool siku ya jumapili.

Kocha Mkuu wa QPR Harry Redknapp ana matumaini timu yake itajiepusha na kushuka daraja msimu huu
Kocha Mkuu wa QPR Harry Redknapp ana matumaini timu yake itajiepusha na kushuka daraja msimu huu
Matangazo ya kibiashara

QPR ambayo ipo mkiani mwa Ligi Kuu nchini Uingereza imeendelea kupambana kujiondoa kwenye eneo hilo licha ya kuandamwa na balaa la kufungwa kwenye michezo yake inayoendelea kwenye kinyang'anyiro cha Ligi Kuu nchini Uingereza.

Redknapp amewaambia wanahabari baada ya mchezo wa kipigo kutoka kwa Liverpool anamatumaini ya hali ya juu timu hiyo haitashuka daraja na badala yake watajiokoa kwenye janga linalowakabili kwa sasa.

Kocha huyo wa QPR amesema pale mnapopoteza mchezo mnastahili kusahau kilichotokea na mnalazimika kujipanga haraka iwezekanavyo kwa ajili ya mchezo ulio mbele yenu kitu ambacho ni muhimu sana kwa kikosi chake.

Redknapp amekiri huenda akalazimika kuingia sokoni mwezi january kwa ajili ya kusajili wachezaji wawili ili kuimarisha kikosi chake akiamini hiyo ndiyo njia nzuri ya kujiondoa kwenye janga la kushuka daraja.

Redknapp ambaye alichukua jukumu la kuinoa klabu hiyo yenye maskani yake huko Loftus Road mwezi Novemba kutoka kwa Mark Hughes amekuwa akipambana ili kujenga kikosi imara lakini kikwazo kikiwa majeruhi.

QPR inakabiliwa na michezo miwili migumu ambayo ni dhidi ya Chelsea na Tottenham michezo ambayo inaweza ikaendelea kutoa mwelekeo wa hatima ya klabu hiyo kwenye kinyang'anyiro cha Ligi Kuu msimu huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.