Pata taarifa kuu
SOKA

Adel Taarabt kutoshiriki fainali za AFCON

Kocha wa timu ya Taifa ya Morocco Rachid Taoussi ametangaza kutomjumuisha Adel Taarabt katika kikosi chake kitakachoshuka dimbani kuwania ubingwa wa michuano ya soka kwa mataifa ya Afrika AFCON itakayoanza kutimua vumbi mapema mwaka ujao.

mirrorfootball.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Taarabt anayekipiga katika klabu ya Queens Park Rangers QPR, ameachwa nje baada ya ombi la Meneja wake Harry Redknapp kukubaliwa na kiungo huyo sasa atabakia nchini Uingereza kuisaidia klabu yake katika michuano ya ligi kuu.

Taarabt mwenye umri wa miaka 23 anatarajia kuisaidia klabu yake katika michezo wanayokabiliana nayo dhidi ya West Ham, Swansea, Manchester City na Norwich.

Michuano ya soka katika bara la Afrika itaanza kutimua vumbi tarehe 19 januari mpaka februari 10 nchini Afrika kusini na Morroco imepangwa katika kundi A ikiwa sambamba na Angola, Cape Verde na wenyeji Afrika kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.