Pata taarifa kuu
SOKA

Kenya yafuzu katika nusu fainali ya mashindano ya kijeshi ya bara Afrika

Klabu ya soka ya Ulinzi Stars ya Kenya imefuzu katika nusu fainali ya michuano ya kijeshi baina ya mataifa ya bara la Afrika baada ya kuishinda Angola mabao 3 kwa 1 katika robo fainali iliyochezwa siku ya Jumatano jijini Abidjan nchini Cote Dvoire.

Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Ulinzi Stars yalitiwa kimyani na mshambulizi Evans Amuoka na kiungo wa kati Stephen Waruru ambaye aliithibitishia Kenya ushindi kwa kuwapa bao la tatu, huku Angola ikipata bao la kufutia machozi kupotia mkwaju wa penalti.

Kenya imeonekana kuwa katika hali nzuri katika mashindano ya mwaka huu licha ya kuanza kwa kusuasua kwa kupata sare ya mabao 3 kwa 3 na Burkinafaso.

Katika mchuano mwingine, Kenya iliifunga Gambia mabao 2 kwa 0 ushindi ambao uliwawezesha kufuzu katika awamu ya robo fainali.

Kenya sasa itemenyana na Mali katika nusu fainali huku wenyeji Cote Dvoire wakimenyana na Cameroon katika nusu fainali ya pili.

Ulinzi Stars inashiriki katika ligi kuu ya Kenya na msimu uliopita ilimaliza ya sita huku ikishinda taji la mwaka 2010.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.