Pata taarifa kuu
SOKA

AI Ahly ya Misri yabanduliwa nje ya kombe la dunia

Klabu ya soka ya Al Ahly ya Misri wawakilishi wa bara la Afrika katika mashindano ya  kuwania taji la klabu bingwa duniani wamebanduliwa nje ya mashindano hayo yanayoendelea nchini Japan baada ya kufungwa na Corinthians ya Brazil bao 1 kwa 0 katika nusu fainali.

Matangazo ya kibiashara

Bao la pekee la Corinthians lilitiwa kimyani na mshambulizi Paolo Guerrero na kuisaidia klabu hiyo kutinga fainali.

Licha ya kuondolewa katika mashindano hayo,mabingwa hao wa soka barani Afrika walionesha kiwango cha hali ya juu cha soka kinyume na ilivyotarajiwa huku wengi wakiona kuwa ndio timu iliyostahili kufika fainali.

Hata hivyo, katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo klabu ya Corinthians ilijaribu kumiliki mchuano huo kakini ikashindwa kutumia nafasi hiyo kufunga mabao.

Kipindi cha pili kilitawaliwa na Al Ahly ambayo ilijaribu kutafuta bao la kusawazisha bila mafanikio huku kiungo wa kati Ahmed Fathi akipoteza nafasi nyingi za kufunga bao.

Kocha wa Al Ahly Hossam El-Badry amesema amehuzuhunishwa mno baada ya kupoteza mchuano huo ambao anasema vijana wake walikuwa na nafasi ya kushinda kutokana na uchezaji wa hali ya juu waliouonesha uwanjani.

Klabu ya Corinthians sasa itacheza dhidi ya Chelsea ya Uingereza au Monterrey FC ya Mexico katika fainali itakayochezwa siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.