Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

John Mikel Obi alimwa faini na chama cha soka nchini Uingereza FA

Chama cha soka nchini Uingereza FA kimetangaza kumpiga faini kiungo wa timu ya Chelsea John Mikel Obi baada ya kubaini kuwa alitoa maneno makali dhidi ya mwamuzi Mark Clattenburg wakati wa mchezo wao na timu ya Manchester United.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa ya chama hicho, imesema kuwa imekubaliana na utetezi wa awali wa Mikel ya kwamba alidhani mwamuzi alimtolea mameno ya kibaguzi wakati akimuelekeza kwanini alimpa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi.

Chama hicho kimemtaka Mikel kulipa faini ya pauni elfu 60 kama adhabu yake ya kutoa maneno ya kejeli kwa mwamuzi wa mchezo huo.

Awali klabu ya Chelsea aliwasilisha malalamiko yake kwenye kamati ya nidhamu ya FA wakitaka kuchunguzwa kwa tukio hilo kabla ya baadae kuondoa malalamiko yao na kukubali yaishe.

Licha ya kukubali yaishe, chama cha waamuzi nchini humo hakikukaa kimya kwakuwa kilitaka kutolewa adhabu kwa klabu ya Chelsea na mchezaji Mikel kwakuwa walimdhalilisha mwamuzi Mark Clattenburg ambaye alichorwa vibaya kwenye vyombo vya habari.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.