Pata taarifa kuu
Uingereza

Raphael Benitez ajipanga kuwaziba midomo mashabiki wa Chelsea

Kocha mpya wa Chelsea Raphael Benitez amesema kuwa atabadili mtazamo wa mashabiki wa timu yake kwani wameonekana kutomkubali inavyotakiwa.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya Benitez imekuja kutokana na mashaki hao kumpokea vibaya na kwa hasira katika mchezo wake wa kwanza tangu kuchukua mikoba ya Roberto Di Matteo.

Kucha huyo amesema kuwa atawanyamazisha mashabiki hao kwa timu yake kufanya vizuri na atahakikisha anafanya kazi kwa juhudi ili timu hiyo ifanye vizuri badala ya kuondoka.

Mashabiki wa Chelsea walichukizwa na matokeo ya kutoka suluhu na Manchester City na kumlumu kocha huyo kuwa hana utofauti wa upangaji wa timu na kocha aliyepita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.