Pata taarifa kuu
Uganda

The Cranes ya Uganda yaanza kujinoa kutetea Kombe la Chalenji

Timu ya Taifa ya Uganda au The Cranes mabingwa watetezi wa kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA maarufu kama Chalenji itaanza mazoezi ya kujinoa mwishoni mwa juma hili tayari kwa maandalizi ya michuano ijayo ambayo itatimua vumbi nchini humo.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kuingia kambini wachezaji 25 walioitwa kikosini watakutana na mashabiki wao katika mafunzo maalumu kwenye uwanja wa KCCA's Lugogo jumamosi asubuhi na baadae jioni wataelekea kambini katika eneo la Mbuya pembezoni mwa jiji la Kampala.

Wachezaji waliopo nje ya nchi akiwemo Emmanuel Okwi anaichezea Simba na Hamis Kiiza anakipiga katika klabu ya Yanga zote za nchini Tanzania watarejea mwishoni mwa juma kujiunga na The Cranes katika kusaka nafasi ya kuutetea ubingwa wao.

Joseph Ochaya anayekipiga katika klabu ya Asante Kotoko ya nchini Ghana atawasili siku ya jumatatu, wakati Martini Kayongo Mutumba wa AIK Stockholm anatarajia kuwasili jumanne ya juma lijalo.

The Cranes walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Chalenji kwa mara ya 12 mwaka jana baada ya kuichachafya Rwanda mabao 3-2 kupitia mikwaju ya penati na sasa wanajinoa ili waweze kutwaa ubingwa kwa mara ya 13.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.