Pata taarifa kuu
Soka

Cote Dvoire timu bora ya soka barani Afrika

Timu ya taifa ya Cote Dvoire inasalia kuwa timu bora ya soka barani Afrika na ya 16 duniani kwa mujibu wa orodha ya hivi punde iliyotolewa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Matangazo ya kibiashara

Algeria ni ya pili na saa 24 baada ya kupanda juu kwa nafasi mbili ikilinganishwa na mwezi uliopita, huku Mali ikifunga tatu bora barani Afrika kiwa ya 27 duniani baada ya kupanda kwa nafasi tano.

Uganda ambayo ni ya 22 barani Afrika ni  ya 90 duniani na ya kwanza katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati ikifuatwa na Rwanda ambayo iko katika nafasi ya 35 na  ya 124 duniani.

Kenya ni ya tatu katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati na 37 barani Afrika na ya 128 duniani, ikifuatwa na Tanzania ambayo ni ya 40 barani Afrika na 132 duniani wakati Burundi ikiwa ya mwisho na kuorodheshwa ya tano na 41 barani Afrika na ya 135 duniani.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni ya 30 barani Afrika na 103 duniani.

Viwango vya soka hutolewa na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kila mwezi na viwango hushuka au kupanda kutokana na mechi mbalimbali zinachezwa wakati wa kipindi cha mwezi mmoja.

Viwango vingine vitataolewa tarehe 7 mwezi ujao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.