Pata taarifa kuu
Simba-Azam

Klabu ya Simba nchini Tanzania yashinda ngao ya jamii dhidi ya Azam kwa mabao 3-2

Ma bingwa wa ligi kuu nchini Tanzania msimu uliopita Simba Sports Club hapo jana imeshinda kombe la Ngao ya jamii ikiwa ni mechi ya uzinduzi wa ligi kuu msimu wa mwaka 2012 kwa kuishinda Azam Sports Klabu mabao 3-2.

wachezaji wa Simba wakisherehekea ushindi
wachezaji wa Simba wakisherehekea ushindi Millardayo.com
Matangazo ya kibiashara

Mashambiki wa timu hizo mbili walikuw awamefurika katika uwanja wa taifa kushangilia mechi hiyo iliokuwa na uwzito mkubwa pande mbili.

Timu ya Azam FC ndio ilioanza kuona langu la Simba katika dakika za mwanzo kabisa za mchezo huo, na kuongeza msumari kabla ya kuelekea mapumziko kwa kupachika bao la pili, ambapo Simba ilirudishwa kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Azam kuunawa mpira kwenye uwanja wa hatari.

Licha ya kufungwa mabao 3-2 na Simba, klabu ya Azam imecheza mchezo mzuri wa kukaba na kushambulia huku wakitumia ufundi mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.