Pata taarifa kuu
Somalia

Matokeo ya mechi za kufuzu kombe la Afrika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini

Vijana wa Leopard wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamejiweka katika nafasi nzuri kuelekea katika kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2013 kwa kuitandika timu ya taifa ya Guinea Ikweta kwa kuzawadia mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika Jumapili 9, 2012.

Jogo da 1° mão em Luanda.
Jogo da 1° mão em Luanda. ANGOP
Matangazo ya kibiashara

Vijana wa timu ya taifa ya Guinea walihitaji sare ya sifuri kwa sifuri hivyo kufaanikiwa kulinda lango kagika kipindhi cha kwanza. Mambo yalibadilika baada ya mapumziko mshambuliaji wa leopards Mbokana alipachika nyavuni bao la kwanza na hivyo kuleta msisimko.
Dakika kadhaa baadae mshambuliaji wa klabu ya Anderlecht nchini Ubelgiji Kasusula akapachika bao la pili kwa kichwa.
Hadi kipenga cha mwisho vijana wa Leopards walishinda mabao 4-0.

Upande mwingine vijana wa Ugnada the Cranes, walishindwa kutamba nyumbani, nakujikuta wamelazimishwa bao 1-0 na Zambia, Vijana wa Lion Indoptables wa Cameroon nao vilevile walishindwa kutamba dhidi ya Cape Verde na kulazimishwa mabao 2-0, huku Nigeria ikienda sare ya kufungana mabao 2-2 na Liberia. Vijana wa Ghana walikuja juu na kuishinda Malawi mabao 2-0, huku Sudan wakitamba mbele ya Ethiopia kwa kuikandamiza mabao 5-0.

Upande wake Cote d'Ivoire iliishinda Senegal mabao 4-2. Zimbabwe imeilambisha mchanga Angola kwa kutandika mabao 3-1
Mechi ya marudio katika mzunguuko huu ni Octoba 12 na 14.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.