Pata taarifa kuu
Uhispania

Ronaldo azua Maswali pengine kuiacha Real Madrid

Mshambuliaji wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amekuwa akizungumzwa sana hii leo na vyombo vya habari kuhusu Mustakabali wake ndani ya timu hiyo, kufuatia kauli yake kuwa hana “raha” ndani ya klabu hiyo.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Christiano Ronaldo
Mshambuliaji wa Real Madrid, Christiano Ronaldo REUTERS/Sergio Perez
Matangazo ya kibiashara

Akiulizwa na vyombo vya habari baada ya mchezo uliofanyika katika uwanja wa Santiago Bernabeu baada ya mchezo ambao uliipa ushindi Real Madrid kwa goli 3-0 dhidi ya Granada hapo jana, kuwa kwa nini hakushangilia akajibu kuwa pengine kwa sababu hakuwa na furaha.

Ronaldo alikuwa mgumu kueleza sababu za kutokuwa na furaha, akijibu kuwa sababu ni za kiweledi zaidi ya sababu binafsi, na kuwa hakuwa tayari kueleza zaidi.

Akiulizwa swali juu ya pengine alikosa furaha kutokana na Mchezaji wa Barcelona Andres Iniesta kupewa taji na UEFA kuwa Mchezaji Bora barani Ulaya,siku ya alhamisi, akajibu kuwa si sababu, sababu ni maswala yaliyo muhimu zaidi, na kuwa Iniesta alistahili taji hilo.

Hali ya kutoshangilia Magoli wakati ya mechi hiyo kulizua hoja katika magazeti mbalimbali kuwa Pengine anataka kuihama Timu hiyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.