Pata taarifa kuu
MAREKANI

Michuano ya US Open yaingia siku yake ya nne

Michuano ya tenisi, ijulikanayo kama US Open inayofanyika huko jiji NewYork nchini Marekani imeingia katika siku yake ya nne huku wachezaji wakiendelea kuchuana vikali. 

Andy Murray mchezaji tenisi upande wa wanaume.
Andy Murray mchezaji tenisi upande wa wanaume. dailymail.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa Wanaume Andy Murry amemcharaza Dodig kwa seti tatu ya 6-2, 6-1, na 6-3 huku Harrisson akimchapa Becker kwa seti tatu za 7-5, 6-4, 6-2 na Tipsarevic kumshinda Ruffin kwa seti tano za 4-6, 3-6, 6-2, 6-3, 6-2.

Na kwa upande wa wanawake, Sharapova amemshinda Dominguez kwa seti mbili ya 6-0, 6-1, na Robson kumpiga Clijsters kwa seti mbili ya 7-6, 7-6 huku Petrova naye akimchapa Halep kwa seti mbili ya 6-1, 6-1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.