Pata taarifa kuu
michezo

Kim Clijsters ameanza vema fainali za michuano ya kimataifa ya Us Open

Kim Clijsters ameanza vema fainali za michuano ya kimataifa ya Us Open kabla ya kustaafu mchezo wa tennis kwa ushindi mnono dhidi ya mpinzani wake raia wa Marekani Victoria Duval.

Kim Clijsters raia wa Ubelgiji atakabiliana na Laura Robson katika mzunguko wa pili
Kim Clijsters raia wa Ubelgiji atakabiliana na Laura Robson katika mzunguko wa pili AFP
Matangazo ya kibiashara

Clijsters, ambaye ameibuka na ubingwa miaka ya 2005, 2009 na 2010,alijiibuka mshindi pia katika mzunguko wa awali wa michuano hiyo kwa seti 6-3 6-1 dhidi ya Victoria Duval mwenye umri wa miaka 16.

Clijsters ambaye ni raia wa Ubelgiji anakabiliwa na Laura Robson katika mzunguko wa pili na itakumbukwa kuwa Laura alimshinda Samantha Crawford.

Wakati huo huo Bingwa mtetezi Sam Stosur alifanya vizuri kama alivyofanya Maria Sharapova na mwenzie Victoria Azarenka .

Mcheza tennis Sharapova, ambaye ni bingwa wa mwaka 2006 hakutatizwa baada ya kumcharaza mchezaji kutoka Hungary Melinda Czink kwa 6-2 6-2,huku katika bingwa wa michuano ya Australian Open na raia wa Belarus akitumia dakika 50 kumlaza raia wa Urusi Alexandra Panova kwa ushindi wa 6-0 6-1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.